Maiti ya mtoto mchanga imekutwa imetumbukizwa chooni huko maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, ilisema kuwa, maiti hiyo ilikutwa ikiwa imetupwa katika choo cha Ronwadi Mwaraku eneo hilo bila mwenyewe kutambua.
Alisema kichanga hicho kinakadiliwa kuwa na umri wa siku moja au mbili na mtu aliyehusika kufanya kitendo hicho hakufahamika mara moja.
Alisema mwili wa kichanga huyo uliopolewa na wananchi kutoka chooni humo na upelelezi wa kina wa kaya hadi kaya unaendelea ili kubaini mtuhumiwa huyo
Thursday, July 1, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nikiwa kama mama nimepatwa na maumivu makali sana. Hivi watu wanawaza nini kwa nini alitafuta mtoto. Hawajua kwamba kuna watu wanatafuta watoto. Inasikitisha sana!!
ReplyDeleteinasikitisha sana!
ReplyDeleteNashindwa kuamini kwamba huyo mwanamke alibeba mimba miezi tisa na kustahimili maumivu ya uchungu kisha kutupa huyo mtoto chooni, nadhani tatizo liko kwenye ubongo. Inaumiza sana.
ReplyDeleteJamani wengine tunalilia watoto wengine wanawatupa EEE Mungu. Huyo mhusika naomba apewe adhabu inastahili maana najua atapatikana tuu.
ReplyDelete