Mwanamke mmoja alitoa kioja baada ya kudai talaka kinguvu huku jamii iliyomzunguka ikimshangaa kwa kilichosemekana kuwa amepata mwanaume mwenye fedha.
Mwanamke huyo, alipokuja kwa wifi yake,kumueleza akamwambie kaka yake ampe talaka kwa kuwa alichoshwa na tabia zake,na kumuamuru akiwa hajampa talaka hiyo ataondoka hata kama hajapewa talaka.
“Mimi namuomba talaka kaka yako hataki kunipa ana maana gani? mimi simuhitaji tena nimechoshwa na dhiki mimi, anipe karatasi langu niondoke nyumbani kwake” na asiponipa naenda bakwata lazima aitoe” alifoka dada huyo kwa sauti bila hata aibu
Wifi huyo alijaribu kumuuliza alikosewa nini na kaka yake huyo, na swali hilo hakutaka kulijibu na kumueleza kuwa yeye anachohitaji ni talaka hahitaji maswali,
Hata hivyo mwanamke huyo ilifahamika na ndugu zake kuwa,alikuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwingine ambaye alimuona atambadilisha kimaisha kwa kuwa ndugu zake hao alidai mwanaume huyo alikuwa na fedha zaidi ya mume wake wa sasa.
Monday, August 9, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nilikuwa nafikiri ni hadithi tu kuwa kuna wanaoa/olewa kwa utajiri. Kaazi kwelikweli ama kweli hilo si penzi la dhati. Duniani hapa kuna vituko
ReplyDelete