Tuesday, October 26, 2010

Bei ya mahindi na maharagwe katika Baadhi ya masoko jijini Mbeya imepanda kutoka Sh 18,000 hadi 20,000 kwa kipimo cha plastiki lenye ujazo wa kilo ishirini.

Uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya msoko ya Ikuti,Mama john,Kalobe,na Mbarizi umebaini kuwa bei zimepanda katika kipindi cha miezi mitatu mfulilizo kutokana na wakulima wengi kutotunza chakula cha akiba katika maghala.

Imebainika kuwa wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakikusanya mazao kutoka kwa wakulima mashambani na kusafirisha nchi jirani ya Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.


Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Mbalizi jijini hapa Tausi Mwambapa alisema awali katika kipindi cha mavuno walikuwa wakinunua ndoo moja ya lita ishirini ya mahindi kwa Sh 2,500 hadi 3,000 kutoka kwa wakulima mashambani.

Pia alifafanua kuwa awali maharagwe kutoka kwa wakulima walinunua Sh 3,000 hadi 3,500 na kwamba sasa wanauza Sh 5,000 kwa mahindi mapya na ya zamani Sh 5,500.

Alisema gunia la ujazo wa plastiki sita linauzwa Sh 33,000 na la ujazo wa plastiki nane linauzwa Sh 44,000.

Alisema maharagwe yamepanda kutoka Sh 18,000 hadi kufikia Sh 20,000 hadi 22,000 ndoo ya plastiki ya kilo ishirini kutokana na ubora wa zao hilo.

Naye Mkulima wa Kijiji cha Iwindi Mbeya vijiini, Josina Samson alisema wamelazimika kupandisha bei ya mahindi na maharagwe mashambani na kwamba sasa ndoo moja ya plastiki ya kilo ishirini kwa Sh 3,000 hadi 3,500.

Samson alisema wamelazimika kupandisha bei ya zao hilo kwa sababu wakulima wengi wameuza mazao kwa wingi kipindi kilichopita na kubakiza akiba ya chakula tu.

“Tulijisahau tukauza mahindi mengi bila kuacha akiba ya kutosha, kuna wakulima wengine hawana chakula cha ziada na sasa wanaanza kununua katika masoko,”alisema.

Mmoja wa wafanyabiashara wa Chakula Mgahawa, Baetus Luwi alisema katika kipindi hiki wako katika wakati mgumu katika bishara kwani wateja wao wakubwa wamekuwa wakilazimika kukimbia kula mboga za majani kutokana na kupanda kwa bei ya chakula katika baadhi ya migahawa.

No comments:

Post a Comment