Friday, April 24, 2009

mtoto aliyeuawa MUSOMA, njaa,umasikini na mfadhaiko ndio chanzo.

mtoto aliyepigwa na baba yake kule Musoma hadi kufa kwasababu ameiba mayai ya Tshs.300, ni kitendo cha ajabu. wengi wamerespond kwenye hii kitu kuwa, ni kwasababu wakurya ndio tabia yao kupiga. Mimi nimekuja na jicho la tofauti, MTOTO YULE ALIIBA KWASABABU ALIKUWA NA NJAA. Baba yake si ajabu alikuwa na mfadhaiko wa maisha magumu.

maisha bora kwa kila mtanzania lini? Kama at least hao wananchi vijijini wangesaidiwa kwa pesa za fisadi mmoja tu, wangefuga kuku wengi wa mayai, baba angemwekea mtoto yule trei kibao ale mayai hadi achoke. KWENYE NYUMBA ZA MAFISADI PAPA, kuna kila kitu(kwa hela za watz), kuna mayai, kuna majuis, manyama, mapochopocho kila kitu. hela hizi zingekuwa kwenye mgawanyo sahihi, kwakweli mtoto yule asingeuawa kwa kuiba mayai nyumba ya pili, angekuwa amekula mayai hadi ameridhika nyumbani. nilishawai kuishi kijijini, wakati mwingine unarudi toka shule unakuta wazazi wameenda shamba hawajaweka msosi, upige deshi hadi jioni. msosi hamna. ndio maana watoto huwa wanaiba kwasababu wanaona njaaa. vita dhidi ya mafisadi pekee ndio itakayoondoa rushwa na ubadhilifu tz ili at angalau mwananchi wa kawaida apate chakula cha kutosha, watoto wetu wasiwe na njaa hadi kufikia kuiba mayai. wazazi wamekuwa na mifadhaiko ya ugumu wa maisha, kina mama wanafariki mahospitalini wakati wa kujifungua, barabara hazijengwi, matatizo kibao. wakati huohuo mafisadi wanajenga mijengo dubai na souzi na ulaya na marekani. hivi watz tutafunguka macho lini, HAWA JAMAA CHINI YA KUMI TU NDO WAMETUZIDI NGUVU, yaani tufisadi tuchache hivi ndo tumeshikilia nchi, watz tumeenda wapi? wametuchukua akili nini? ati, kina rostam, manji na wenzao wametuchukua akili? sasa mbona hata wakati mengi na wengine wamejitoa muhanga sisi bado tunatoa mimacho tu? tuandamane hawa jamaa kama sio waaminifu waadibishwe. huku mtaani watu njaa na matatizo yamewazidi kwasababu yao.
ITS A RIGHT TIME NOW FOR THE GOVERNMENT TO ACT!!...
WE PEOPLE ARE SICK AND TIRED OF THIS MAFISADI SONG!!

No comments:

Post a Comment