Thursday, May 21, 2009

Afa wakati akitoa maelezo kituo cha polisi.

Mkazi wa Yombo Kilakala ,Philemon Mtonga (52) amefariki dunia wakati akiendelea kutoa maelezo katika kituo cha polisi.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Temeke, Rukia Simbakalila amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3 asubuhi katika kituo cha Chang’ombe.

Amesema Mtonga alianguka ghafla kituoni wakati akiendelea kutoa maelezo ya awali katika kituo hicho.
Amesema alifuatana na mke wake kituoni hapo na wakati akiendelea kutoa maelezo yake ghafla alidondoka chini na kukimbizwa hospitalini kumbe alikuwa ameshafariki.
Amesema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa inadhaniwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Kamanda huyo alisema kabla ya kifo chake mtu huyo alikuwa akitoa maelezo kituoni hapo ya kuwa mtu mmoja alikuwa akimtishia maisha.

Amesema kwa bahati mbaya kabla hajamaliza maelezo yake hayo alianguka na kufariki papo hapo.
Awali ilidaiwa wakati wa uhai wake marehemu alishawahi kupigiwa simu toka mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume kumtishia kuwa kesi zote alizomsingizia alishinda na kumwambia kuwa sasa atampa kesi ya ubakaji, kilisema chanzo cha habari kituoni hapo.

Amesema hata hivyo upelelezi unaendelea kufanyika kuhusiana na tukio hilo ili kugundua chanzo cha kifo hicho kwa undani.

No comments:

Post a Comment