Thursday, May 21, 2009

anazaa kila mwaka tangu alipokuwa na miaka 15.

Mwanamke mmoja nchini Uingereza anazaa karibia kila mwaka tangia alipokuwa na umri wa miaka 15, hivi sasa ana umri wa miaka 24 na ana jumla ya watoto saba na tayari ana mimba ya mtoto wa nane.
Susie Christian mkazi wa mji wa Norwich nchini Uingereza hivi sasa ana umri wa miaka 24 na alianza kuwashangaza wazazi wake wakati alipopata ujauzito wa kwanza alipokuwa na umri wa miaka 15.
Susie aliwashangaza zaidi wazazi wakati huo pale alipokabidhiwa mtoto wake kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua na kusema anataka kuzaa watoto wengi zaidi.
Katika miaka tisa Susie amejifungua jumla ya watoto saba na hivi sasa ana mimba ya mtoto wa nane.
Kutokana na kwamba Susie hafanyi kazi na mumewe naye hana kazi, Susie anapokea jumla ya paundi 24,000 ( takribani Tsh. milioni 48 ) kwa mwaka kama msaada wa malezi ya watoto wake hao kutoka serikalini.
"Watu waache kunisema sana kwa kuwa naishi kwa msaada wa serikali, hakuna kazi nzuri duniani kama kuwa mama wa nyumbani" alisema Susie.
Mama huyo kijana alisema kwamba pamoja na kutokuwa na uwezo wa kuwanunulia watoto wake kila kitu wanachokitaka, anaishi maisha ya furaha na watoto wake.

No comments:

Post a Comment