Friday, May 22, 2009

waislamu wapigana na polisi waliochana Quran.

Waislamu nchini Ugiriki wamepigana na polisi nchini humo waliokuwa wakivunja maandamano yao kufuatia taarifa kwamba polisi walimpiga muislamu mmoja na kuuchanachana msahafu aliokuwa ameubeba na kisha kuvikanyaga kanyaga vipande vya msahafu huo.

Waislamu wapatao 1500 waliandamana jijini Athens jana baada ya taarifa kuwa polisi walimpiga muislamu waliyemkuta na msahafu kwenye begi lake na kisha kuuchanachana msahafu huo na baadae kuruka ruka juu ya vipande vya msahafu huo waliouchana.

Waandamanaji hao ambao wengi wao walikuwa ni wahamiaji toka Syria na Afghanistan waliandamana kuelekea kwenye kituo cha polisi cha Kypseli kilichopo kwenye eneo ambalo linaongoza kwa kuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu jijini Athens.

Polisi walijaribu kuyavunja maandamano hayo na kusababisha vurugu kubwa ambazo ziliisha kwa polisi kutumia mabomu ya machozi.
Waandamanaji hao walisema kwamba siku ya jumatano maafisa wa polisi wa Ugiriki waliwasimamisha wahamiaji wanne toka Syria kucheki uhalali wao kuwepo nchini humo.

Katika kuwasachi wahamiaji hao, polisi hao walikuta msahafu katika begi la mmoja wa raia hao wa Syria na ndipo walipoanza kumpiga huku wakiuchana msahafu huo.

Polisi hao inasemekana baada ya kuuchana msahafu huo waliruka ruka juu ya vipande vya msahafu huo vilivyokuwa vimezagaa chini.
Polisi wa Ugiriki hawajasema chochote kuhusiana na tukio hilo la kuchwanwa kwa msahafu.








No comments:

Post a Comment