Saturday, May 23, 2009

Akutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia shuka.

Mkazi mmoja wa Buguruni Shaba Salum amekutwa amekufa huku mwili wake ukining’inia kwenye kenchi la chumba chake alimokuwa akiishi.

Kamanda wa Ilala, Faustine Shilogile alisema kuwa mwili huo ulikutwa juzi jioni eneo la Buguruni Malapa.Alisema mtu huyo alijinyonga kwa kutumia shuka ambayo alijitundukia kwenye kenchi zake za chumbani.

Amesema chanzo kilichopelekea kifo hicho bado hakijajulikana na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Amana.
Katika tukio jingine amesema nyumba moja iliyopo maeneo ya Yombo imeungua kwa kuteketea kwa moto.

Amesema chanzo cha kuungua nyumba hiyo ni mshumaa ambao uliachwa katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo na kupelekea moto huo.
Amesema hadi sasa haijajulikana thamani ya nyumba hiyo vikiwemo na mali zilizoteketea kufuatia moto huo.

No comments:

Post a Comment