Monday, May 18, 2009

bweni la wanafunzi lamliza Naibu Waziri.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini, Bi.Mwantumu Mahiza, mwishoni mwa wiki iliyopita alilazimika kutoa machozi mbele ya kadamnasi baada ya kufanya ziara katika shule ya Sekondari ya wavulana ya Zingibari iliyopo mkoani Tanga.

Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya kushtukiza ya kukagua shule hiyo ambapo alikuta wanafunzi wakiishi katika hali mbaya sana ikiwemo uchakavu wa mabweni.
Alikuta wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo wakiishi katika nyumba chakavu ya makuti.

pichani juu ni jengo ambalo ni bweni la wanafunzi hao!
bweni hili lina uwezo wa kubeba wanafunzi wapatao 25.

1 comment:

  1. hii hali sio siri,inatisha!!
    haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania kweli?
    i dont think so!kama shule zenyewe ndio zipo hivi...inasikitisha.

    ReplyDelete