Monday, May 18, 2009

Mbwana Matumla apigwa-Philippines.

Mbwana Matumla 'Golden Boy' usiku wa kuamkia jana ameshindwa kuwika nchini Philippines mbele ya bondia wao AJ 'Bazooka' Banal baada ya kupewa makonde mazito yaliyomfanya aliage pambano hilo kwa Knockout katika raundi ya pili.

Kabla ya pambano hilo Matumla alikuwa gumzo nchini humo kutokana na historia yake nzuri katika ndondi akionekana ni tishio kubwa kwa bondia huyo wa Philipines.

Katika pambano hilo lililofanyika kwenye mji wa Cebu nchini Philippines, AJ Banal al maarufu kama "Bazooka" alilitawala pambano hilo akimpa makonde Matumla kuanzia dakika ya kwanza ya mpambano.

Matumla ambaye alionekana dhahiri kuelemewa na mfilipino huyo katika raundi ya pili, ilimbidi aliage pambano hilo katika raundi hiyo baada ya kupewa makonde mawili mazito yaliyompeleka chini.

Matumla alijaribu kuamka bila mafanikio na ndipo refa wa pambano hilo alipoamua kumaliza pambano hilo katika raundi ya pili dakika ya 2:59.

Kutokana na ushindi huo,Banal amefanikiwa kupata nafasi ya kuzipiga kwenye usiku wa mpambano wa kukata na shoka kati ya Mmarekani Floyd Mayweather na Juan Manuel Marquez julai 18 jijini Las Vegas.

No comments:

Post a Comment