Sunday, May 31, 2009

Ilala Yatwaa Kwa Mara nyingine Taifa Cup.

Timu ya Ilala imefanikiwa kutetea ubingwa wake katika Taifa Cup baada ya kuitandika Temeke 1-0 katika mechi ya fainali na kufanikiwa kujishindia kitita cha Tsh. milioni 30.

Timu ya Ilala leo imetetea ubingwa wake wa kombe la Kili Taifa Cup kwa kuinyuka timu ya Temeke bao moja kwa bila katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa ni wa vuta nikuvute ukiwa umejaa ufundi wa kutosha kwa kila timu.
Walikuwa ni Ilala waliofanikiwa kuona lango la mwenzake kunako dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Salumu Pakala ambaye alifunga goli hilo kwa ufundi baada ya kumvika kanzu kipa wa Temeke Dida.

Kutokana na ushindi huo kwa miaka miwili mfululizo timu ya Ilala imejinyakulia zawadi ya mshindi wa kwanza kiasi cha Shilingi Milioni 30 na kikombe.

Temeke ambao ni washindi wa pili wamejinyakulia kiasi cha Shilingi Milioni 15.
Mshindi wa tatu Timu ya Tanga Shilingi Milioni 7.5 na mwanza ambayo imenyukwa leo na Tanga kwa mabao 2 -0 imejinyakulia kiasi cha shilingi milioni 3.

Mfungaji bora wa mashindano hayo ni Athumani Idd chuji ambaye amefungana na mchezaji wa Temeke wote wakiwa wamefunga mabao matano.

Ilala imeweka historia ya kuwa timu ya kwanza kulitwa kombe hilo mara mbili mfululizo chini ya Kocha wake mkuu Julio ambaye leo amekuwa kocha bora na kuzawadiwa kiasi cha shilingi milioni 2.

No comments:

Post a Comment