Saturday, May 30, 2009

watu wawili wajeruhiwa katika ajali ya Hiace dar.

Watu wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Kimara Baruti baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuingia kwenye mtaro wa kandokando barabara ya hiyo

Ajali hiyo iltokea jana usiku majira ya saa 3 wakati gari hilo lilipokuwa likijaribu kumpita aliyekuwa mbele yake.
Hivyo wakati akijaribu kufanya zoezi hilo na gari lililokuwa mbele yake kuelekea upande wa kushoto zaidi na gari hiyo kushindwa na kujikuta linaingia mtaroni.
Kwenye Hiace hiyo kulikuwa na watu wapatao tisa wakiwa wanatokea Ubungo kuelekea Mbezi.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo abiria wakishirikiana na wasamaria wema wengine waliofika kutoa msaada walimpa kichapo cha nguvu dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo na baadae kumfikisha katika kituo cha polisi kilichokuwa karibu na eneo hilo.

Majeruhi hao waliweza kuchukuliwa na raia wema na kukimbizwa zahanati iliyo karibu kwa kuangaliwa hatua za awali.

No comments:

Post a Comment