Tuesday, May 12, 2009

Maghembe Azomewa mbele ya Museven-UDSM.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe azomewa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mbele ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kile kilichodaiwa kukerwa na utendaji wa Waziri huyo.
Tukio hilo lilitokea jana katika uzinduzi wa kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii chuoni hapo.

Kuzomewa kwa Waziri huyo kumekuja baada ya kuwasili kwa wageni rasmi watarajiwa na wakati lilipofika zoezi la kutambulisha wageni hao katika ukumbi wa Nkuruma.

Wageni wote waliotambulishwa walishangiliwa na wanafunzi hao lakini ilipofika muda wa kutambulishwa kwa Waziri huyo mwenye dhamana ya elimu nchini wanafunzi hao walimzomea waziri huyo na kuzuka fujo ukumbini hapo.

Kuzomewa kwa Waziri huyo kulipelekea ratiba ya shughuli hiyo kuvurugika na kufanya Makamu Mkuu wa UD. Prof. Rwekaza Mukandala ashike dhamana ya kumkaribisha Rais Museven ili kuepusha kusitisha fujo hizo.

Baadhi ya wanafunzi hao waliohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini kutaka kutoa sababu ya kumzomea kiongozi huyo walidai kuwa Waziri huyo imekuwa ni kichocheo kikubwa cha migogoro kutokea na kutorishidhwa na maamuzi yake toka ashike madaraka hayo.

Walisema Waziri huyo amefanya migomo ya hapa na pale kutokea na kutojali maslahi ya wanafunzi hao na kujinufaisha mwenyewe na kutojali wanyonge na vilevile kuwafukuza wanafunzi wa chuo hicho na kutaka kujisajili upya.

Suala la mikopo ya elimu ya juu imekuwa ni vikwazo, hali kutokuwa shwari vyuoni hata mashuleni, malalamiko ya walimu yakiongezeka na kutotimiziwa malalamiko yao na uvujaji wa mitihani wa mara kwa mara “hali inayofanya kuboa kwenye Wizara hiyo na aachie madaraka” walisema wanafunzi hao.

FOR MORE:

1 comment:

  1. NIKWELI BODI YA MIKOPO IMEKUA IKIENDESHWA KIBABE BILA KUJALI MASLAHI YA RAIA WA HALI YA CHINI

    ReplyDelete