Wednesday, May 6, 2009

TAKUKURU na mafisadi,ni chanda na pete!

Inashangaza kusikia/kuona kuwa sasa Rostam badala aende mahakamani alikoshauriwa kwenda kwa lengo la kujisafisha mbele ya jamii ya watanzania, yeye amekimbilia TAKUKURU.

Je kuna nini huko? kwa nini anakimbilia huko?

Huko TAKUKURU ndio kule shauri la Richmond lilipopelekwa, lilisafishwa kabisa.Ndio huko huko ambako mkurugenzi wake hashikiki ingawaje amekwishashutumiwa kwa mambo kadhaa.

TAKUKURU ilikuwepo Dr. Slaa alipotaja majina ya mafisadi lakini ilikaa kimya hadi moto ulipozidi ndio wale walaji wa EPA walipopekwa Kisutu.
TAKUKURU isiyo na meno, ambayo Rostam anaijua vizuri kwamba haina mpango wa kuwabana makada wa CCM na hasa maswahiba wa rais ndio sasa Rostam anapeleka malalamiko na uthibitisho kwamba Mengi ni mkwepa kodi na madeni ya mabenki.

Rostam anajua wazi kuwa kufanya hivyo TAKUKURU haitahangaika na ukweli ulioko katika madai kwamba yeye ni fisadi papa na ya kwamba amewahujumu watanzania yeye binafsi.

Rostam anajua wazi kuwa anaiweka TAKUKURU busy kushughulika na eti madai dhidi ya Mengi na lazima ofisi yetu hiyo ambayo sisi walala hoi tunaigharamikia kwa kodi nyingi itajifanya blind dhidi ya uovu wa Rostam na kupoteza muda mwingi kumchunguza Mengi halafu wanaamini kuwa temperature ya madai dhidi ya mafisadi papa itapoa tu yenyewe.

tusubiri tuone TAKUKURU itampa tafu gani bwana Rostam,bearing in mind kwamba ndio mfadhili mkuu wa CCM.

2 comments:

 1. Haya mambo ni magumu sana ndugu yangu. Sababu ya Rostam kukimbilia takukuru ipo lakini kwa mtanzania wa kawaida ni ngumu sana kutambua.

  Nilisoma Gazeti la raia mwema toleo no 80, ilikuwa ni ishu hii hii ya Rostam na Mengi, mwandishi aliuliza swali hili "inakuwaje wakati Lowasa alipotuhumiwa kwa ufisadi na hata Mkapa, Sofia simba na viongozi wengine hawakuwatetea na wakati leo hii wanamtetea Rostam? Nadhani kuna jambo hapa.

  Kimsingi ni kwamba watanzania tulio wengi hatujui kinachoendelea, tupo giyani, tunasikiliza malumbano,yaishe, yasiishe, tunaona sawa tu, yani hatuna patriotism kama vile viongozi wetu wasivyo na patriotism pia.

  ReplyDelete
 2. NYINYI MSIOJUA HII VITA NI MAFISADI WANAGOMBANIA MASLAHI BINAFSI SIO MENGI WALA SIO ROSTAM NA WAHINDI WENZIE WOTE WEZI WAKUBWA.
  MENGI AMEKUA NA HISTORIA NDEFU SANA YA KUANZISHA VITA NA WATU AMBAO WAMEONEKANA KUTISHIA MASLAHI YAKE BINAFSI NASIO YA TAIFA.
  NADHANI KAMA MMEKUA WATU WAKUFATA DATA ZIPO,HUA ANAPENDA KUTUMIA MWAMVULI WA UZELENDO NA KUTUMIA UMASKINI TULIO NAO WATANZANIA KUJINUFAISHA BINAFSI.
  AMEKUA AKITUZALILISHA WANANCHI WA HALI YA CHINI KWA KUTUPAKA MAFUTA KWA MGOGO WA CHUPA,HIVI LEO IKITOKEA KENMPYSK INAUZWA HIVI NI WATANZANIA WANGAPI WAZALENDO WATAKAO WEZA KUINUNUA?ZAIDI LA TABAKA LA WACHACHE LAKINA MENGI NA HAO WAHINDI NDIO WATAOWEZA KUMUDU,JE SISI MAKABWELA TUTAFAIDIKA NA NINI JUU YA MENGI KUNUA ZABUNI HIZO ZAIDI YA YEYE NA FAMILIA YAKE KUZIDI KUJILIMBIKIZIA MALI.
  MUDA MREFU MENGI AMEKUA AKITUMIA VYOMBO VYAKE VYA HABARI KUPANDIKIZA PROPAGANDA ZAKE,KUJITANGAZA NA KUFANIKISHA KUFANYA UFISADI WAKE!!NA KUANZA KUJIONA KAMA MUNGU MTU NA NDIOMAANA SERIKALI IM%ETUMIA BUSARA KUKEMEA HILI SUALA.

  SERIKALI ILIKUA INASUBIRI KUPATA MWANYA WA KUKEMEA MWENENDO AMBVAO MENGI ALIKUA ANAENDA NAO NA KUAMBUKIZA VYOMBO VYA HABARI VYENGINE NCHINI VIKIWEMO VYA HUYU FISADI MWENZIE ROSTAM!!TUMESHUHUDIA VIKIFANYA USHABIKI WA HALI YA JUU.
  ILA TUSISAHAU KWAMBA MADHARA YA HIVI VYOMBO VYA HABARI KIUSALAMA KAMA SERIKALI INGEMWACHIA MENGI NA WENZIE KUENDELEA BILA KUHESHIMU MISINGI YA UANDHISHI NA UMILIKI WAKE INGEKUJA KUA HATARI KWA TAIFA LETU,TUMESHUHUDIA NCHI ZA JIRANI MFANO RWANDA NA BURUNDI VYOMBO VYA HABARI VILIVYOCHUKUA NAFASI KUBWA KULETA MAAFA.
  WEWE KAMA NI MTANZANIA MZALENDO HUTOTEA MAFISADI.
  ALICHOKIFANYA ROSTAM NI SAWA KWANI KESI KAMA HIZI HUWEZI KUMPELEKA MTU MAHAKAMANI BILA KUA NA PROVE INGAWA NAE NI FISADI VILEVEILE.
  VITA VYA MAFISADI SISI KWETU NI FURAHA KWANI TUTANUFAIKA SANA TU KWA TAIFA LETU KUTOLIWA.
  TUWAACHE WAFIKISHANE KWENYE VYOMBO HUSIKA.
  ME NADHANI KAMA UMEKUA MFATILIAJI WA DATA HUWEZI KUMTETEA MENGI AMA ROSTAM WOTE NI WEZI WAKUBWA

  ReplyDelete