Monday, May 4, 2009

Tanzania Broadcasting Corruption(TBC1) inapotumika vibaya.

TBC wanaoendeshwa kwa kodi yako wewe na mimi. Hawa ndio waliotumiwa na Rostam Aziz kuihusisha kwa nguvu zote CHADEMA na Kifo cha Wangwe. Mnaweza kukumbuka mtiririko wa mambo waliyoyafanya. Hawa ndio waliokatisha hotuba ya Dr Slaa kuhusu ufisadi aliyotoa bungeni watanzania wasiione. Ndio hao hao, wiki iliyopita walikatisha hotuba ya Zitto Kabwe iliyohusu ufisadi. Hawa ndio ambao leo wamerusha maelezo ya fisadi Rostam Aziz(wenyewe wanasema kwa kulipia). Kwa hiyo natoa hoja, Dr Slaa peleka TBC ule mkanda wako wa hotuba yako ya Mwembe Yanga. Ule ambao TBC hata kwenye habari yao hawakurusha majina ya mafisadi badala yake walisema tu 'wapinzani wataja watuhumiwa wa ufisadi'. Sasa peleka mkanda mzima, wewe ni mbunge kama Rostam Aziz. Rusha hewani hotuba yako yote ya mafisadi 11. Kama walivyoirusha hotuba ya leo ya Fisadi Rostam Aziz. Hiyo ndio Tanzania Broadcasting Corruption(TBC). Halafu wakaulizwe Sophia Simba na Mkuchika, kuhusu utawala bora na matumizi ya vyombo vya habari.

1 comment:

  1. Nice blog but i cant understand the language :(

    ReplyDelete