Tuesday, June 30, 2009

mama mjamzito afariki Kwenye Mabenchi ya Mapokezi ya hospitalini Dar.

Mama mmoja aliyekuwa ni mjamzito amefia kwenye mabenchi ya mapokezi katika zahanati moja iliyotambulika kwa jina la M. Tatu iliyoko maeneo ya Mwananyamala kisiwani jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamanda mkoa wa Kinondoni, Sebastian Masinde amesema kuwa tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana majira ya saa 3 asubuhi katika zahanati hiyo.
Amesema mama huyo alikadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na alikuwa na mimba isiyopungua umri wa miezi sita.
Kamanda Masinde alisema kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa na madaktari kwenye zahanati hiyo umeonyesha kuwa mama huyo alikuwa akikabiliwa na matatizo ya upungufu wa damu.
Masinde aliendelea kusema kuwa mama huyo alitakiwa aende kwenye hospitali ya serikali ili akapate huduma nzuri huko.
Mama huyo kwa kuwa alikuwa hajisikii vizuri alikwenda kukaa kwenye mabenchi hayo na kufariki hapo.
Mwili wa mama huyo umechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment