Thursday, July 2, 2009

Nusu nauli kwa wanafunzi yasitishwa

Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imesitisha mpango wa wanafunzi kulipa nusu ya nauli ya mtu mzima kwenye mabasi ya daladala, mpango huo ulitarajiwa kuanza jana.
Ongezeko la nauli hizo zilizowataka wanafunzi hao kulipa nusu ya nauli ya mtu mzima kwenye mabasi uliotarajiwa kuanza leo uliotangazwa na Mamlaka hiyo wameusitisha hadi hapo watakapotangaza tena.
Mkurugenzi wa Sumatra, Israel Sekirasa alisema kuwa nauli ya shilingi 100 kwa wanafunzi itaendelea kutumika kwa mabasi yote ya daladala hapa nchini hadi itakapotangazwa rasmi.
Kusitisha kwa nauli hizo kumetokana na kutoa nafasi kwa wadau wa usafiri kujadili kwa kina juu ya uanzishwaji wa nauli hiyo na kuandaa mazingira mazuri ya utekelelezaji huo.
Hivyo Mamlaka hiyo imetaka wamiliki wa mabasi nchini kuendelea na nauli ya zamani na si iliyotangazwa awali na kinyume na hapo atakayelipisha nauli iliyositishwa atachukuliwa hatua.

Baaadhi ya wazazi waliohojiwa na mtandao huu jana wamefurahia sana uamuzi ulitolewa na Sumatra kwa kuwa umewakomboa wanyonge na walikuwa wanahofia sana juu ya kuongezeka kwa nauli hizo kwa wanafunzi.

Walikuwa wanaiomba mamlaka hiyo kuendelea kusitisha nauli hiyo tarajiwa ili iwakomboe mana wanaweza wakajikuta watoto wanashindwa kwenda shuleni kutokana na uchumi kuwa mgumu.

No comments:

Post a Comment