Thursday, July 2, 2009

TopLand hoteli yateketea kwa moto

Ile hoteli inayojulikana kwa jina la TopLand iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam imeteketea kwa moto.
Hoteli hiyo iliungua kwa moto jana na kusababisha upotevu wa mali zilizokuwa katika hoteli hiyo.
Chanzo cha habari kilisema kuwa moto huo ulianza ghafla katika ghorofa ya pili ya jengo hilo na hatimaye moto kusambaa katika baadhi ya ghorofa nyingine za hoteli hiyo.
Habari hizo zilisema kuwa chanzo kilisemekana ni moshi ulianza kutoka kwenye mashine ya kiyoyozi.
Hivyo kutokana na kuzuka ghafla kwa moto huo mteja mmoja aliyekuwemo katika moja ya chumba katika hoteli hiyo alikuwa anakimbia hovyo na kujikuta amegongwa na gari kwa ajili ya hofu na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Hata hivyo uongozi wa hoteli hiyo ulisema bado hawajapata tathimini kamili juu ya hasara iliyopatikana katika hoteli hiyo.

No comments:

Post a Comment