Sunday, June 28, 2009

Polisi Wamhoji daktari wa Michael Jackson.

Polisi wa Marekani wanajiadaa kumhoji daktari binafsi wa Michael Jackson ambaye alikuwa naye wakati alipofariki baada ya kuchomwa sindano yenye dawa ya kutuliza maumivu.
Michael Jackson inasemekana alifariki muda mchache baada ya kuchomwa sindano ya dawa ya kutuliza maumivu yenye nguvu sana Demerol.
Polisi walimhoji Dr Conrad Murray, daktari binafsi wa Michael Jackson aliyekuwepo nyumbani kwake wakati anafariki muda mfupi baada ya kifo cha Michael Jackson lakini walielezea mpango wao wa kumhoji kwa urefu zaidi daktari huyo.
Maafisa wa polisi walilichukua gari la Dr Conrad kutoka kwenye nyumba ya Michael Jackson ili kulifanyia uchunguzi kama linaweza likawa na madawa au vitu vyovyote vitavyosaidia kutoa ushahidi wa kifo cha Michael Jackson.

Hata hivyo polisi walikanusha taarifa kwamba wana mpango wa kumhoji mshauri wake wa pili wa masuala ya afya Dr Tohme R Tohme, ambaye aliambatana na Michael Jackson hadi hospitali baada ya kuzidiwa siku ya alhamisi.
Taarifa mbali mbali zimekuwa zikitolewa kwamba Michael Jackson aliyefariki akiwa na umri wa miaka 50 alikuwa akitumia mchanganyiko wa madawa mbali mbali ya kutuliza maumivu yenye nguvu sana.
Deepak Chopra, daktari wa madawa ambaye alikuwa rafiki wa muda mrefu wa Michael Jackson alielezea jinsi alivyokuwa akimshauri Michael Jackson kuhusiana na utumiaji wake mbaya wa madawa ya kutuliza maumivu yenye nguvu sana tangia mwaka 2005.
Chopra alisema kuwa mara ya mwisho kuongea na Michael Jackson kuhusiana na utumiaji wake wa madawa yenye nguvu sana ilikuwa ni miezi sita iliyopita.
Chopra alisema kwamba Michael alimuomba dawa ya kutuliza maumivu yenye nguvu sana ya Oxycontin mwaka 2005 wakati Michael Jackson alipokuwa akikaa kwake wakati wa kesi yake ya kuwanyanyasa watoto kijinsia.

Chopra alisema kuwa alikataa kumpa dawa hiyo lakini Michael Jackson alilalamika na kumwambia "Hujui ni kwa jinsi gani ninavyosikia maumivu".
Chopra alimalizia kwa kusema kuwa siku zote alipoanzisha mada ya utumiaji wa madawa bila mpangilio, Michael Jackson alikuwa akiikwepa mada hiyo.

Michael Jackson alianza kutumia madawa ya kutuliza maumivu miaka kadhaa iliyopita wakati nywele zake ziliposhika moto wakati wakitengeneza tangazo la video la Pepsi.

1 comment: