Wednesday, June 24, 2009

wauza madawa ya kulevya dar.

Jeshi la Polisi nchini limeanza msako wa kuwasaka madereva tax ambao wanajihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya kwa wageni waingiao nchini.
Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dare s salaam, Suleiman Kova alipokuwa anatoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.
Kova amesema kuwa Jeshi hilo limeanza msako mkali kwa kuwa wamebaini kuwa baadhi ya madereva tax wanajihusisha na biashara hiyo jijini.
Amesema madereva hao wamekuwa wakijihusisha kuuza madawa hayo ya kulevya kwa wageni mbalimbali wanaofika nchini katika mahoteli mbalimbali na kusababisha vifo vyao.
Ameongeza kuwa, katika kipindi cha mwezi mmoja jumla ya wageni watatu kutoka nje ya nchi waliofika hapa nchini kwa shughuli zao mbalimbali wamekufa baada ya kutumia madawa hayo waliouziwa na maderea tax hao.
Amesema wamebaini kuwa madereva wanaoegesha magari yao kwenye mahoteli mbalimbali jijini wamekuwa wakijihusisha na uuzaji wa dawa hizo kwa wageni hao.

Hivyo msako mkali unaanza kufanyika kuwabaini madereva wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuwachukulia hatua.

No comments:

Post a Comment