Monday, July 6, 2009

achomwa moto mpaka kufa.

Kijana mmoja ameuawa kwa kuchomwa moto baada ya kutaka kujaribu kupora na kuiba gari ndogo aina ya Toyota alilokodi huko maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo alifika katika kituo cha tax cha Tegeta majira ya saa mbili za usiku na alitaka kukodisha gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Shabani.
Alimuamrisha dereva huyo ampeleke maeneo ya Mbezi Beach na dereva huyo alianza safari ya kumpeleka mteja wake huyo alikotaka kwenda.

Punde wakati anakaribia maeneo hayo ya Mbezi Beach kutokea Tegeta kijana huyo alimuamrisha dereva huyo asimamishe gari na alilipora na kukimbia nalo.
Dereva huyo mara moja alitoa taarifa kituo cha polisi na kuwaambia baadhi ya wenzake na kuanza kulikimbiza gari hilo na kufanikiwa kumpata maeneo ya Mbezi Beach akiwa amekwama njiani wakati amegonga gari nyingine ndogo.

Ndipo walipomkamata kijana huyo na kujichukulia sheria mikononi na kumchoma kwa moto hadi walipohakikisha amekufa kila mtu aliondoka kivyake.
Wakati askari polisi walipofika eneo la tukio walimkuta tayari mtu huyo ameshafariki dunia na kuuchukua mwili wake na kuupeleka sehemu husika kuuhifadhi.

No comments:

Post a Comment