Monday, July 27, 2009

Ajali ya basi. Lori yaua zaidi ya watu 30 Tanga

Zaidi ya watu 30 wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Mohammed Trans, kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kupitia Nairobi nchini Kenya, kupata ajali wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, zinasema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa gurudumu moja la basi hilo na kugongana uso kwa uso na gari la mizigo aina ya Scania, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Arusha.

Hadi tunakwenda hewani, ni majeruhi 13, ndio waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe, Magunga, mkoani Tanga na katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, iliwekwa taa ya kandili kutokana na kukosekana kwa umeme ili shughuli za kuweka miili ya marehemu hao ziendelee .
Habari zaidi zilisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kwa Kombo wilayani Korogwe, majira ya saa moja jioni jana.

Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya alisema hadi muda huo kulikuwa na maiti 27 zilizokwisha patikana, wanaume 21 na wanawake sita.
Wakati huohuo, mtu mmoja amefariki dunia katika ajali iliyotokea maeneo ya Wami mkoani Tanga baada ya gari la Kampuni ya Airbus lililokuwa likisafiri kwenda Dar es Salaam jana kugongana na lori.

No comments:

Post a Comment