Sunday, July 26, 2009

Nyama, maharage mekundu hatari kwa afya

nyama nyekundu hasa ya ng’ombe, pamoja na maharage mekundu ni sababu kubwa zinazosababisha magonjwa ya magoti na viungo.
Sababu nyingine zinazo sababisha ugonjwa huo, ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa pamoja na kutofanya mazoezi.

Hayo yamesemwa juzi na Mtaalam wa Mifupa na Viungo wa Hosptali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam Dk Sohail Panawala alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Tofauti na imani ya watu wengi kuwa nyama ya Mbuzi ndiyo husababisha magonjwa ya miguu, Dk Panawala alisema, “Ulaji wa nyama nyekundu na hasa nyama ya Ng’ombe uwezekano wa kuwa na matatizo ya miguu ni mkubwa sana,”.

Mtaalam huyo ambaye toka aingie nchini mwezi Februari mwaka huu, ameshafanya upasuaji kwa zaidi ya wagonjwa 100 na wengine wengi kupatiwa matibabu yasiyo husisha upasuaji.
Alisema kutokana na ukubwa wa tatizo la miguu na viungo nchini, mara kadhaa hulazimika kuwa na kliniki ya bure ya mifupa na miguu, ili kutaka kubadilishana mawazo na wagojwa pamoja na matibabu.
Dk Panawala pia alionya juu ya matumizi ya madawa ya kupunguza maumivu, kuwa ni hatari na kuwa huzalisha magojwa mengine.
“Unajua madawa yote yana kemikali na kawaida ya kemikali huwa na madhara (side effect) katika mwili wa binaadamu, tatizo la watu kutumia madawa ya kupunguza maumivu lipo duniani kote lakini ni bora mtu ukiumwa mara moja aende hospitalini ama katika kituo cha afya apate matibabu,” alisema Dk Panawala.
Hospitali hiyo ya Aga Khan pia, imefanikiwa kuwafanyia upasuaji wa ubongo, zaidi ya wagonjwa 20 kwa kipindi cha miezi minne.
Mbali na wagonjwa hao, waliopatiwa fanyiwa upasuaji pia wagonjwa wengine zaidi ya 200, wamefanyiwa vipimo mbali mbali vikiwemo vya ubongo na uti wa mgongo.

No comments:

Post a Comment