Monday, July 20, 2009

jamani hospitali ya mwananyamala kuna mambo!

Mwanamke mmoja alijikuta yupo kwenye wakati mgumu baada kugundua kuwa amebadilishiwa mtoto wake aliyejifungua kutoka hospitali na kuondoka na mtoto sio wake.
Chanzo cha habari kimedai kuwa mwanamke huyo alifika katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kujifungua.
Tukio hilo la kubadilishiwa mtoto kwa mama huyo lilitokea leo asubuhi.
Inadaiwa kuwa mama huyo alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike ambaye alimfurahia kwa kuwa alikuwa na watoto wa kiume watatu mfululizo.
Wakati mama huyo alipojifungua mtoto huyo wa kike alimpigia mumewe simu akimtaarifu kuwa amejifungua mtoto wa kike.
Hivyo manesi waliokuwa wanamsaidia walimkabidhi mama huyo mtoto wake na kumuhakikishia kuwa alikuwa wa kike.
Hivyo katika pilika pilika katika wodi hiyo ya wazazi haijulikani ilikuwaje alijichanganya wakati gani wa kupima kilo za mtoto huyo na kuchukua mtoto si wa kwake ama alibadilishiwa wakati alipokwenda msalani ama ilikuwaje aliweza kubadilishiwa mtoto huyo bila kujitambua.

Muda wa kuruhusiwa uliwadia na mama huyo kumbeba kichanga wake kwa ajili ya kuanza safari kuelekea nyumbani.
Ndugu walifika na kumchukua mama huyo, wakati wapo ndani ya tax kabla ya kuanza safari mmoja wa waliokuja kumchukua kuelekea nyumbani alimfunua mtoto huyo kwa ajili ya kumuangalia ndipo walipogundua tofauti hiyo.
Ndipo mama huyo aliposhuka na kuelekea sehemu za wodi za wazazi huku akilia kwa uchungu na makelele hadi kupelekea kutokuelewana kwa watu waliokuwa karibu na eneo hilo la tukio.

“Nimebadilishiwa mtoto wangu nimechukua sio wa kwangu, nitafanyaje jamani na nitamwambia nini mume wangu nitaonekana muongo mimi” alilalama mama huyo.
Chanzo cha habari kilisema kuwa aliwaelezea manesi na kuanza taratibu za kuhakiki upya kwa kuwauliza wazazi kama kuna mwingine aliyechukua mtoto sio wake.

Hadi tunakwenda mitamboni ilikuwa bado haijajulikana kama mama yule alifanikiwa kupata mtoto wake ama la.

No comments:

Post a Comment