Monday, July 20, 2009

Kina Klothing Yafungua Duka MtandaoniSalaam kwa wadau wote blogu ya hii samvande.
Kina Klothing ina furaha kuwafahamisha kuwa imefungua duka lao mtandaoni na unaweza sasa kununua Tshirt moja kwa moja kupitia http://www.kinaklothing.com/
Kina ni kampuni mpya ya nguo ambayo inawakilisha Bongo na Afrika kwa ujumla. Kwa utambulisho imetoka na kollektion inayoitwa Uhuru St. kwa sababu neno uhuru linabeba sababu nzima ya sisi kuanzisha Kina.
Vilevile hii ni lebo ya mavazi ya kitaa na Uhuru ni mtaa wa kwanza katika mfululizo wa kollektion zitakazobeba majina ya mitaa mbalimbali ya Bongo na Afrika kwa ujumla.
Kama kauli mbiu yao inavyosema “Vitu vyetu. Kivyetu” basi ndio wanavyotarajia kuendesha lebo yao, yaani full uhuru wa kutengeneza kazi zinazotuwakilisha, kwa namna tunayoamua wenyewe.
Tshirt hizi zimesanifiwa mahsusi kwa ajili ya wabongo na marafiki zao ili kuonyesha kuwa wabongo nao tumo katika medani hii ya design; lakini si hivyo tu, ujumbe unaobebwa na nguo kina ni mchango wetu katika harakati za kujenga madaraja kati ya waafrika barani na diaspora kwa kusambaza na kusheherekea yale yanayotuunga pamoja kama waafrika.
Hata hivyo, katika kollektion hii ya kwanza wameamua “kucheza kwetu” zaidi, tunatumai utatutunza.
Watembelee www.kinaklothing.com na utoe maoni yako.
au kutana nao kwenye ukurasa wao wa facebook
(http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819) na kutufuatia katika http://www.twitter.com/kinaklothing
Kaa mkao wa kula kwa kollektion inayofuatia, Samora avenue. Iko jikoni


No comments:

Post a Comment