Friday, July 17, 2009

kero za nyumba za kupanga

Kero na karaha za nyumba za kupanga zimejidhirisha huko maeneo ya Mikocheni B baada ya mama mwenye nyumba kuvitoa vitu vyote vya mpangaji wake ambaye alikuwa safarini na kisha kuigeuza nyumba aliyokuwa amempangisha kuwa kanisa.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rose ambaye alikuwa amepanga katika nyumba namba 104 iliyopo katika mtaa wa Nyumbu Mikocheni B, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mwenye nyumba wake kumtolea vitu vyake vya thamani nje huku yeye akiwa safarini hajui sakata hilo.
Rose alimuanga mama mwenye nyumba yake aliyefahamika kwa jina la Joyce Mbunga kuwa anakwenda Mbeya kwa ajili ya matibabu ya mwanae anayesoma mkoani Mbeya ambaye alikuwa ni mgonjwa.
Mtoto huyo alikuwa amevunjika miguu na alipelekwa hospitali ya Wemba Mission ya Mbeya. Kutokana na hali ya mtoto huyo kutoridhisha walitakiwa wampeleke mtoto huyo hospitali ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Wakati mama huyo akiwa Mbeya akihangaikia matibabu ya mwanae, mama mwenye nyumba alikuwa akimpigia simu akimtaka aje atoe vyombo vyake katika chumba alichopangishwa.

Rose akiongea na mwandishi wa habari hizi alisema tayari walikuwa na makubaliano ya kupanga katika nyumba hiyo ambapo kwa muda wa miezi minne tayari alikuwa amesha mlipa mama mwenye nyumba hiyo kiasi cha shilingi elfu 40000.

Hata hivyo mama mwenye nyumba hiyo alipata wateja wengine waliopenda kupanga katika eneo hilo kwa nia ya kufanya kanisa.
Wakati mama huyo akiwa bado safarini mama mwenye nyumba alivitoa vitu vyote vya mpangaji wake na kuviweka nje na kisha kuipangisha nyumba yake kwa watu walioigeuza kuwa kanisa ambao inasemekana si raia wa Tanzania.
Nyumba hiyo iligeuzwa kanisa linaloitwa KANISA LA KIMATAIFA LA LIGHT HOUSE CHAPEL likiwa na ujumbe unaosema THE MEGA CHURCH ( KANISA KUBWA).

Rose baada ya kurudi na kukuta vitu vyake vyote vikiwa nje huku vingine wezi wakiwa wameishajichukulia na nyumba hiyo imeishageuzwa kuwa kanisa alisikitika sana na kutoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba 10 ambaye alikiri kitendo cha mama mwenye nyumba si cha kiungwana.
Kesi hiyo ilifika kituo cha polisi Oysterbay na mama mwenye nyumba ameshawekwa ndani.

1 comment: