Friday, July 17, 2009

'Mtoni' maisha magumu sana-mwanaFA

Msanii maarufu wa Bongo Flava Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ambaye alienda nchini Uingereza kusoma amerudi Tanzania na kusema maisha ya ulaya ni magumu sana na watu wanateseka sana. Mwana FA hawashauri watu waache kazi zao Bongo kukimbilia ulaya.

Siku chache baada ya kudondoka kutoka pande za Uingereza anakopiga kitabu, mkali wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA amesema amejionea kwa macho yake baadhi ya watu wanaoishi huko wakitaabika bila kuwa na ishu ya kufanya.
Msanii huyo alisema kwamba, baadhi ya vijana wengi bado wana ndoto za kwenda Ulaya wakidhani kwamba maisha ni rahisi kitu ambacho siyo cha kweli kwakuwa huko pia wapo watu wengi wasiokuwa na ajira wanasota mitaani.
“Ulaya maisha magumu washkaji, mtu kama una dili yako ya kupata miambili miambili Bongo bora utulie uendelee kuongeza kipato na kuijenga nchi yako badala ya kukimbilia Ulaya.

Ninachoongea watu wanaweza wasiniamini lakini anayeweza aende akajionee mwenyewe,” alisema FA ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya, ‘Nazeeka sasa’ iliyowashirikisha Prof. Jay na Sugu.
FA.Aidha, mchizi aliiambia safu kuwa, mwishoni mwa mwezi huu atarudi Uingereza kwa ajili ya kumalizia masomo yake ambapo anatarajia kukusanya mafaili yake na kurudi Bongo Desemba mwaka huu akiwa na Masters yake.

No comments:

Post a Comment