Saturday, July 11, 2009

Obama Aanza Ziara Yake Ghana.

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili jijini Accra, Ghana kwa ziara yake ya siku moja ikiwa ni ziara yake ya kwanza kusini mwa jangwa la Sahara tangu kushika madaraka ya urais.
Polisi 10,000 walijipanga nchini humo kuhakikisha ulinzi wakati wa ziara hiyo ya rais wa kwanza mweusi wa Marekani.
Rais Obama alipokelewa na mwenyeji wake rais wa Ghana John Atta Mills na atalihutubia bunge la Ghana baadae leo.
Katika hotuba yake katika bunge hilo, Rais Obama anatarajiwa kueleza maoni yake kuhusu uongozi mzuri na maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.
Baadae Obama na mkewe Michelle na watoto wake watatembelea mji wa Cape Coast ambao ulikuwa kituo kimojawapo cha kuwachukua watumwa kutoka Afrika na kuwasafirisha hadi Marekani.
Obama amechagua kwenda Ghana kwa ziara yake ya kwanza katika katika kanda hiyo kwa sababu nchi hiyo imetajwa kuwa ni mfano mzuri wa utulivu na maendeleo ya kidemokrasia barani Afrika.

Ghana ilipata uhuru mwaka 1957 na baadae ilikumbwa na mapinduzi ya kijeshi na tangia mwaka 1990 Jerry Rawlings aliporuhusu mfumo wa vyama vingi nchini humo vyama vya upinzani vimeshinda uchaguzi mara mbili.

No comments:

Post a Comment