Monday, August 31, 2009

Apigwa risasi akiwa Grosari Dar

Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo kwa kupigwa risasi ya tumbo na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi akiwa anakunywa kinywaji grosari huko Kimara jijini Dar es Salam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Mark Kalunguyeye amesema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi, majira ya jioni huko Kimara Kilungule katika grosari moja inayojulina kwa jina la Grace.

Amesema kuwa mauaji hayo yalitokea mara baada ya watu hao kuvamia grosari hiyo na kumpiga risasi ya tumboni marehemu huyo.
Amesema mtu aliyeuawa katika tukio hilo alitambulika kwa jina la George Magere (38).
Mara baada ya tukio hilo watu hao waliondoka na kutomdhuru mtu mwingine na kutoiba kitu chochote katika grosari hiyo na chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika.
Amesema polisi mkoa wa Kinondoni wapo kwenye juhudi za kuwasaka watu hao na kuwakamata.

No comments:

Post a Comment