Friday, August 7, 2009

Mama akamatwa na dawa za kulevya.

Mama mmoja mkazi wa Nairobi nchini Kenya amekamatwa na kilo 3 za dawa za kulevya aina ya Heroine katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mwanamke huyo alikamatwa alipofika katika stendi hiyo akitokea nchini Kenya kupitia Tanzania kwa ajili ya safari yake ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini.
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Bw. Godfrey Nzowa amesema kuwa mwanamke huyo wamemkamata katika stendi hiyo ya Ubungo ambapo madawa hayo aliyaficha katika mfuko wake alipoweka nguo zake.
Amesema mwanamke huyo alikuwa anatokea nchini Kenya akisafiri kuelekea nchini Afrika ya Kusini kupitia Tanzania Zambia.
Mwanamke huyo baada ya kukamatwa na madawa hayo ya kulevya alifikishwa kituo cha polisi na kufunguliwa mashitaka.
Mwanamke huyo alikutwa na hati ya kusafiria iliyokuwa na namba 1732 iliyotolewa mjini Nairobi Kenya.
Nzowa amesema kuwa mwanamke huyo anaendelea kushikiliwa na polisi na hatua za kumfikisha mahakamani zinachukuliwa.

No comments:

Post a Comment