Thursday, August 6, 2009

Muuguzi kutoka Marekani , Lee Ann Falls akimpima mmoja wa watoto waliojitokeza katika kliniki ya bure iliyoandaliwa na Shirika la Afya na uokoaji (Chara) iliyofanyika katika kijiji cha Tondooni kisiwani Pemba hivi karibuni. Wakazi wa kijiji hicho walipatiwa misaada mbalimbali ya chakula na matibabu ya bure kwa wakinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano, pamoja na vyandarua ili kujikinga na malaria.


Magari yakikwepa shimo lililochimbwa kwenye barabara ya Azikiwe,Posta Mpya Dar es Salaam,huku likiwa limejaa maji taka yaliyokuwa yakitoa harufu kali na ya kutisha.

No comments:

Post a Comment