Friday, August 21, 2009

Miss Tanzania kufanyika 3/10/2009.

Warembo watatu kuziba nafasi za mrembo wa Uingereza, Schengen na Songea katika shindano la miss Tanzania mwaka huu litakalofanyika Oktoba 3 Jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Miss Tanzania alisema kuwa kwa mwaka huu hakutakuwa na Miss Tanzania UK, kutokana na kutofanyika kwa shindano hilo na nafasi yake itazibwa na Gloria William kutoka Ilala huku nafasi ya Miss Schengen nayo haikufanyika kutokana na mshindi Leila Ally kutokizi vigezo hivyo itazibwa na Easter Gao kutoka Miss Vyuo vikuu na mrembo Gloria Nicholas kutoka Ruvuma hatoweza kushiriki kwa sababu za kimasomo na nafasi yake kuzibwa na Witness Nesphory kutoka Mkoa wa Iringa.
Alisema warembo hao wanatimiza idadi ya warembo 30 watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo kwa mwaka huu kutoka kanda mbali mbali hapa nchini .
Lundenga alisema kuwa kambi ya warembo hao wataitangaza hivi karibuni kwani bado wanamalizia maandalizi na yote ni kuhakikisha kuwa warembo wanakaa kwenye kambi nzuri na yenye hadhi ya juu.

No comments:

Post a Comment