Saturday, August 1, 2009

vibaka wazidi manzese darajani.

Wananchi waishio maeneo ya Manzese darajani wameitaka Manispaa kuimarisha ulinzi katika daraja hilo kwa kuwa vibaka wameweka kambi eneo hilo.
Wakazi hao waliitaka manispaa kuimarisha ulinzi katika daraja hilo kwa kuwa wezi na vibaka wamekuwa wakijificha na kutishia maisha ya wakazi wa maeneo hayo.


Wamesema wezi hao hujificha katika daraja hilo na hupora mali za watu pindi wapitapo darajani hapo.
Wamesema kuwa nyakati za usiku vibaka wamekuwa wakijificha darajani humo hali inayofanya wakazi kuogopa kulitumia daraja hilo na kuvuka njia ya kawaida chini na kusababisha idadi ya ajali kuongezeka.
Wakazi wa maeneo hayo wameiomba manispaa kuweka walinzi kwenye daraja hilo kwani daraja hilo litakuwa halina faida kama wakazi wa eneo hilo wataendelea kuogopa kulitumia kwa kuhofia kukabwa na wezi wanaowasubiria watu kwenye daraja hilo.

No comments:

Post a Comment