Wednesday, September 30, 2009

CUF kuandamana kupinga Tume ya uchaguzi

Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) jijini Dar es Salaam, leo wanatarajiwa kufanya maandamano ya amani kushinikiza kuundwa tume huru ya uchaguzi.

Imedaiwa na baadhi ya wanachama wa CUF wamedai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyopo sasa, imeshindwa kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki tangu iundwe miaka 17 iliyopita.
Maandamano hayo yanayotarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, yataanzia katika eneo la Sheli, Buguruni, jijini Dar es Salaam saa 4:00 asubuhi na kuishia katika ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini zilizoko katikati ya jiji.Profesa Lipumba amesema wameamua kufanya maandamano hayo kupinga taratibu zinazoendeshwa na tume hiyo kuwea inaendeshwa isivyo halali.

Profesa Lipumba pia, alisema uamuzi wa serikali wa kuchapisha karatasi za kupiga kura bila kuwashirikisha wadau, vikiwamo vyama vya siasa kuhusu usalama na mawazo mengine, ni wa hatari kwa vyama hivyo.
Naye Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alipotakiwa kuzungumzia maandamano hayo alisema, ingawa maandamano hayo ni jambo la halali lakini hayuko tayari kupokea maandamano hayo ya CUF kwenye ofisi yake kwa vile eneo hilo ni nyeti na linazungukwa na ofisi nyeti.

No comments:

Post a Comment