Wednesday, September 16, 2009

Maofisa BOT Kizimbani kwa kuhujumu Uchumi.

Maofisa 4 wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jana wamefikishwa katika mahakamani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhujumu uchumi wa nchi.

Watuhumiwa hao ambao ni wakurugenzi wa benki hiyo ni Bosco Kimela, Simon Jengo, Kisima Mkango na Ally Bakar walifikishwa katika Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi Samweli Maweda.
Kesi hiyo ilikuwa ikiongozwa na Mwendesha Mashitka kutoka Taasii ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Beni Rinkolini na kudai kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka yapatayo matatu likiwemo la kuhujumu uchumi.

Rinkolin alidai kuwa washitakwia wakiwa watumishi katika benki hiyo walimdanganya mwajiri wao mnamo mwaka 2004 kwa kuandaa rasimu ya ziada kwa wasambazaji wa noti ya mkataba ya wmaka 2001 kwa lengo la kudanganya.

Alidai kuwa mshitakiwa wa kwanza mwaka 2005 aliagiza kuchapishwa kwa noti kwa thamani kubwa ya fedha kinyume na ile iliyopangwa na BOT.
Aliendelea kudai kuwa washitakiwa hao wote kwa pamoja walishindwa kutekeleza majukumu yao wakiwa watumishi katika benki hiyo kwa kuandaa rasimu ya ziada iliyoonyesha thamani kubwa ya kuchapisha kiwango cha noti kuliko mkataba uliosainiwa na benki hiyo mwaka 2001.

Kutokana na sheria za nchi washitakiwa hao walikosa dhamana na wamerudishwa mahabausu na watarudishwa tena mahakamani Septemba 18, mwaka huu kwa kutajwa.

No comments:

Post a Comment