Tuesday, October 6, 2009

3% ya watanzania wana matatizo ya macho

Zaidi ya asilimia tatu ya Watanzania wanakabiliwa na matatizo ya uono hafifu huku asilimia moja wakiwa hawaoni kabisa.
Takwimu hii ilitolewa jana na Mratibu wa Taifa wa Huduma ya Macho wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Nkundwe Mwakyusa katika maadhimisho siku ya afya ya macho yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa watanzania walio wengi wanakabiliwa na matatizo ya macho na bila kufatlia afya ya maco na katika watu waliojitokeza katika upimaji wa macho wamegundua kuwa walio wengi wanakabiliwa na matatizo hayo. Hivyo Dk. Mwakyusa amesema kutokana na hali hiyo ameitaka jamii kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mashujaa-Mnazi Mmoja kupatiwa huduma ya macho bure katika wiki hili la kuazimisha afya ya macho ambayo kilele kitakuwa Octoba 8 mwaka huu.

Amesema watanzania wajitokeze kw wingi katika viwanja hivyo na kwa ajili ya kupimwa macho na kupatiwa matibabu bure na endapo atagundulika kuwa tatizo la mgonjwa ni kupatiwa miwani atapatiwa bure.
Amesema wka waliopima waliowengi wamegundulika na tatizo la mtoto wa jicho ambalo linaathiri kwa asilimia 50 ukungu katika kioo cha jicho ambalo huathiri kwa asilimia 20, ukoma katika jicho (asilimia 10) pamoja na magonjwa mengineyo kama vile kisukari, presha ya jicho na mengine.

Alisema wamepanga kuzitumia siku hizo nne kutoa huduma ya macho kwa wananchi bure hivyo aliwataka wananchi kuzitumia siku hizo kupatiwa huduma ya macho na kwa watakaokutwa na tatizo watahudimiwa bure.

No comments:

Post a Comment