Wednesday, October 7, 2009

Mali za Mil. 15 zaibwa bodi ya Mikopo

Mali za shilingi Milioni 15 zimedaiwa kuibwa na watu wasiofahamika waliovamia katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyopo Msasani
Imedaiwa kuwa majambazi hao kwa kushirikiana na walinzi waliokuwa lindo walivamia ofisi hizo kisha kukomba mali zote ikiwemo kompyuta ya sekretari wa ofisi hiyo ambayo ilikuwa na kumbukumbu muhimu.Chanzo kimedaiwa kuwa pia majambazi hao walivamia katika ofisi za Mkurugenzi wa bodi hiyo na kuiba kompyuta aliyokuwa akiitumia.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na lilitokea majira ya saa 12 asubuhi, na kusema kuwa jeshi lake linaendelea na upelelezi zaidi.Amesema katika tukio hilo walinzi wawili waliokuwa lindo wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.Alisema kuwa majambazi hao wameiba komyupta 10 aina ya Dell zenye thamani ya sh.milioni 15.

No comments:

Post a Comment