Tuesday, October 27, 2009

Magari yenye thamani ya Mil 445 yateketea kwa moto

Moto mkubwa umezuka katika kiwanda cha nondo cha Metro Steel, Kiwalani cha jijini Dar es Salaam na kusababisha kuteketeza yadi ya kuuzia magari iliyokuwa karibu na kiwanda hicho cha kuuzia magari aina ya Faw na kuteketeza magari yenye thamani ya Sh m 445.

Kamanda wa Polisi wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:15 usiku ambapo alisema chanzo cha moto ni ulizuka kwenye kinu cha kuyeyushia vyuma.

Kamanda Shilogile alisema wakati ufuaji ukiendelea kiwandani hapo, mlipuko mkubwa ulitokea na kuenea hadi eneo la jirani katika yadi ya kuuza magari ya Kampuni ya J.F Track & Equepment ambapo uliteketeza magari tisa mapya aina ya Faw yenye thamani hiyo ya fedha.

Moto huo ulikuja kuzimwa na Kikosi cha Zimamoto cha Jiji na hakuna madhara kwa binadamu yaliyotokea.Amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzid zaidi juu ya chanzo cha moto huo na taarifa itatolewa pindi uchunguzi utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment