Monday, October 5, 2009


Maji yakiwa yamejaa katika mitaa ya Sheikh Amin kutoka na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko jijini Mwanza jana.

1 comment:

  1. Wala sishangai japo kila siku nasikia wakisema kuwa MWANZA INAKUA. Yaani ukuaji wa mTanzania mimi ni ule wa muonekano tu. Hakuna la ziada. Haya majengo yanayojengwa kwa kasi hayaendani na uboreshaji wa mifumo ya majitaka. Yaani maji machafu na vyoo sijui vikianza kufurika Dar tutawaeleza nini wale tuliowakaribisha kuwekeza. Angalia Mwanza. Mvua ikinyesha kidogo tunasikia maafa. Sio mafuriko tu, hata maradhi kwani watu milimani hawana vyoo na serikali inaendelea kusema huko waliko si mahala pa kuishi na SHIRIKA LAKE LAENDELEA KUGAWA UMEME HUKO.
    Nchi ya kitu kidogo.
    Lakini naisikitikia Tanzania yangu INAYOJENGA GHOROFA NA KUPUUZA UBORA WA MSINGI kama nilivyoandika hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/09/tanzania-yangu-ijengayo-ghorofa-bila.html

    Blessings

    ReplyDelete