Friday, November 13, 2009

Shabiki mmoja wa soka wa nchini Uingereza ambaye alikuwa jukwaani mwishoni mwa wiki iliyopita kushuhudia Chelsea ikitoa dozi kwa Manchester United (Mashetani wekundu) kwenye mpambano wa ligi ya Uingereza, amewaacha watu wengi wakiwa na maswali mengi kuliko majibu baada ya kunaswa live akipiga mswaki uwanjani kama vile yuko nyumbani kwake.

Shabiki huyo wa soka ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alionekana vyema wakati Salomon Kalou na Michael Owen walipokuwa wanajiandaa kuingia uwanjani kutokea benchi kwenye kipindi cha pili cha mechi hiyo ambayo Manchester ililala kwa bao 1-0 lililofungwa na nahodha wa Chelsea John Terry.

No comments:

Post a Comment