Sunday, April 11, 2010

7 wafa, 10 wapofuka macho-kenya.

Pombe ya kienyeji maarufu nchini Kenya kama Chang'aa imesababisha vifo vya zaidi ya watu 7 na kupofuka macho kwa watu wengine 10.

Zaidi ya watu saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 10 wamebaki vipofu baada ya kunywa pombe maarufu nchini Kenya kwa jina la Chang'aa.
Wakazi wengi wa kitongoji cha Shauri Moyo jijini Nairobi nchini Kenya walikimbizwa hospitali wakiwa hawajiwezi baada ya kunywa Chang'aa (Gongo).

Katika tukio hilo lililotokea jana, watu watatu walifariki kwenye eneo la tukio wakati watu watano walipofuka macho hapohapo baada ya kubwia kilevi hicho cha kienyeji ambacho ni kinyume cha sheria kukutwa nacho.

Mkuu wa kituo cha polisi cha Buruburu alisema kuwa watu wengi zaidi waliwahishwa kwenye hospitali ya Kenyatta baada ya kunywa pombe hiyo.

Baada ya kunywa pombe hiyo, watu walianza kutoa mapovu mdomoni huku wakilalamika maumivu makali ya tumbo.


Hadi kufikia leo watu waliopoteza macho yao wamefikia 10 huku jumla ya watu 7 tayari wameishapoteza maisha yao.

No comments:

Post a Comment