Mbunge wa Bahi mkoani Dodoma,CCM bwana Omar Badwel amesomewa maelezo ya awali kuhusu kesi inayomkabili katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam, kesi inayomkabili ya kuomba na kupokea rushwa.
keshi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa rasmi tarehe 6 mwezi wa nane mwaka huu kwa upande wa mashahidi wa Jamhuri wapatao 16 watakaoanza kutoa ushahidi wao.
katika hatua za awali, mbunge huyo amekiri jina lake, anuani yake, na kuwa yeye ni mbunge wa jimbo la Bahi na kuwa yeye ni mjumbe wa kamati za hesabu za serikali za mitaa (LAAC).
Pamoja na hayo, mbunge huyo amekata maelezo yaliyosomwa na wakili wa serikali, Lizy Kiwia kuwa mei 30 mwaka huu alimpigia mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mkuranga Sipora Liana kupitia namba ya simu +255784858855 na yeye akitumia namba +255789089189 akimjulisha kuwa wajumbe wa kamati ya LAAC wanakutana na kumtaka na kumtaka aje kesho yake kwani mambo siyo mazuri kwa upande wake.
Pia mbuneg huyo alikatana kumweleza Liana kuwa wajumbe hao wanakutana june 4 mwaka huu jijini dar es salaam na Liana kumweleza kuwa hatoweza kuja siku hiyo kwa sababu ana kikao kingine katika manispaa yake hivyo waonane juni 1 mwaka huu.
Mshitakiwa huyo alikana kuomba rushwa ya shilingi milioni 8 kutoka kwa mkurungenzi huyo wa wilaya ya mkuranga.
Mshitakiwa huyo pia alikana kukamatwa juni 2 mwaka huu katika hoteli ya peacock iliyopo jijini dar es salaam akipokea rushwa ya shilingi milioni 1 kutoka kwa mkurungenzi huyo wa wilaya ya mkuranga ili kuwashawishi wajumbe wa kamati hiyo waweze kupitisha taarifa yake ya fedha ya mwaka 2011/2012.
Tuesday, July 17, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment