Chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali kuu ya mkoa wa Shinyanga kimeungua moto leo majira ya asubuhi.
Moto huo ulianza ghafla ndani ya chumba hicho baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme na kupelekea kutokea kwa hasara kidogo ya baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani ya jengo hilo.
Taarifa imedai kuwa, hakuna mtu yeyote aliyedhurika wala maiti iliyoteketea kwa moto kwa kuwa ndani ya chumba hicho kulidaiwa kulikuwa na maiti moja tu ya mtoto ambayo pia ilidaiwa haikupata madhara kwakuwa iliwahiwa kuokolewa.
No comments:
Post a Comment